Zanzibar
televisheni, ndo televisheni ya
kwanza
tena yenye kuonyesha picha za rangi. Televisheni hii ndo ilikuwa ya kwanza
katika bara la Afrika kusini mwa Sahara. Ilikuwa ikimilikiwa na taifa na niayake ilikuwa nikuleta maendeleo kwa kutumia vipindi vyake.
Ilianza mwaka 1972 na ilikuwa inarushwa kwa Kiswahili na kingereza pia ilibeaba vipindi vya ndani na vya kimataifa.
Ilipatikana katika maeneo mbali mbali kama kwenye visiwa vya Unguja na Pemba, pia signal
zake zilifika hadi Dar es salaam,
Tanga, Bagamoyo pia hadi Mombasa Kenya.
Niaya televisheni ya Zanzibar
ilikuwa kuelimisha, kuburudisha na kutoa habari. Iliitwa
“Televisheni ya kuelimisha” kutokana na wazo
la Raiswa Zanzibar
wakati huo ambaye alikuwa Marehemu Abeid
Amin Karume.
Baadaya
Zanzibar
televisheni huku bara ikanzishwa televisheni nyingine iliyoitwa ITV(Independence Television)
ilioanza rasmi mwaka 1994 wakati wa kombe
la dunia. Na
baadaya hii televisheni ikaanzishwa televisheni nyingine ambayo ilikuwa inamilikiwa na taifa iliyoitwa Televisheni ya Taifa
(TVT). Hii ilianza kuonekana rasmi mwezi machi
2000 baada ya kumalizika kwa ujenzi wa kituo pale
kijitonyama jijini Dar es
salaam. Badae TVT(TelevisheniyaTaifa) ikabadilishwa na kuitwa TBC
ambalo jina hilo linatumika hadi sasa.
Vilevile kuna vituo vingine vingi viliazishwa ambavyo ni vya binafsi na vingine vya jamii ambavyo vimeanzishwa katika miji mbali mbali nchini ambavyo hurusha matangazo ya ndani na kutoka nje ya
Tanzania kwa Miktaba Maalum.
Pamoja na kuwa na televeshini zetu wenye bado tuna
changamoto kubwa kwa mfano bado kuna maeneo mengine kama vijijini haya na huduma ya televisheni.
Pia sehemu nyingine zinatumia ungo ilikupata televisheni hizi.Hii ni changa moto kubwa kwa vyombo vya habari haswa television.
Licha ya televisheni pia kuna vyombo vingine vya habari ambavyo vilianzishwa kama Redio yaTaifa
(RTD). Hii Redio Tanzania inausikivu
85 katika eneo la
nchi la kilomita za mraba 93970.
Pia chombo kingine ni magazeti ambayo mpaka sasa ni magezeti 350
yaliyo sajiriwa lakini 15
tu ya machapisho hayo ambayo yana onekana mitaani kwa wakati huu.
Idadi kubwa ya magazeti yaliyo sajiliwa yana milikiwa na watu au
kampuni binafsi. Ila “Daily News”
na “ Sunday News” zinamilikiwa na Serekali chini ya Uongozi wa kampuni ya magazeti ya Serekali
(Tanzani Standard Newspaper Limited).
Vyombo vyote vya habari bado vina changa moto kubwa katika kutumikia watu wake
na nchi kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment